Agano la Krismasi

Zawadi yetu ya Tumaini

Muundo sawa wa kanda Ulimwenguni

Kanisa kwa wote kwa huduma Pamoja

 

Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni ninyi kwa ninyi kwa mapendo. Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu. Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja. Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja; kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote. Waefeso 4: 1-6

 

Kwa neema ya Mungu sisi sote ni sehemu ya Mwili wa Kristo, tunashauriwa kupendana kama vile Mungu alivyotupenda. Hata katika hali ya sintofahamu kanisani mwetu na ulimwenguni kwa jumla, twahimizwa kwa Injili ya Yesu Kristo ambayo inatoa uponyaji, upendo, na maridhiano kwa wote. Tunahimizwa kusherehekea wingi wa neema ya Mungu, kuthibitisha misingi yetu ya kikristo kama Ubatizo, kutambua tofauti za karama zetu za kiroho na huduma, na kushiriki kwa uaminifu katika utume wa Mungu kwa pamoja. Kama vile John Wesley alitamka kabla ya kujiunga na wingu kubwa la mashahidi, "zaidi ya tote, Mungu yu pamoja nasi!" Hakika, hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu na kati yetu.

Maono yetu:

Kama United wamethodisti wa kanda ya kati, maono yetu ni kuwa na Kanisa linalounganisha mataifa, kujishughulisha katika huduma pamoja, kuheshimu mipangilio ya muktadha na kuaadhimisha utofauti wa uumbaji wa Mungu kwa maneno mengi mazuri, na maadili kwa pande zote kuwezesha husiano ili kuimarisha dhamira yetu na misingi ya uinjilisti, Ufuasi, na ushuhuda kwa mataifa yote kwa mnajili ya kuwafanya watu kuwa wafuazi na mabadiliko ya ulimwengu. Hili ndio agano letu.

Mwongozo na kanuni zetu:

Mtazamo wetu umeegemezwa kwa kanuni zifuatazo zipendwazo na jamii yetu ya ulimwengu na United wamethodisti wa kanda ya kati. Hizi kanuni zinatuhimiza kufikiria upya kuwa Mwili wa Kristo katika ulimwengu wa leo:

Sisi sote ni watoto wa Mungu

Kanuni zetu za kijamii za kanisa la United Methodist yanakili , "Tunaamini kuwa kitambulisho chetu cha msingi ni kuwa sisi ni watoto wa Mungu. … Kanisa linataka kukumbatia kikamilifu na kukuza malezi ya kitamaduni na uwezo kama njia ya kuwa mwili mmoja kamili, ulioonyeshwa kwa njia nyingi ”(2016, ¶161.A) Kuzingatia undugu wengine wa kimo na usawa wa haki ni dhamana muhimu ya kibinadamu iliyohifadhiwa na Imani yetu ya Kikristo. "Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu. ” (Wagalatia 3:28). Kwa kuthamini tofauti zetu kama sawa, ni Agano takatifu kwetu - lililotiwa nanga kwa neema - kushiriki na wengine uhuru wa kushiriki Injili kulingana na muktadha wetu wa kimisheni.

Ubuntu

 Ubuntu ni wazo la Kiafrika ambalo linajumuisha njia ya maisha ambapo ubinadamu ni msingi wa uelewaji na kutegemeana kwa maisha ya jamii. Imewekwa kwa kugundua kuwa sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na tunapaswa kuwafanyia wengine kama tunataka ifanyike kwetu. Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini asema, "Ukweli mkubwa ni kwamba, huwezi kuwa mwanadamu peke yako. ... Wewe ni binadamu kwa sababu unashiriki katika uhusiano. Inasema mtu ni mtu kupitia watu wengine. Hii ndio tunasema. Hii ndio Biblia inasema. Hii ndio kile uzoefu wetu wa kibinadamu hutufundisha. "

Bayanihan

Bayanihan ni dhana nzuri ya kale ya Wafilipino ya ushirikiano wa jamii nakufikia malengo ya jamii. Neno bayan, linamaanisha taifa au jamii, bayanihan tangu jadi imeonekana kwa msaada halisi wa jamii kwa familia ambazo zinahitaji kuhama. Watu wenye kimo wa barrio hubeba mbao nzima za nyumba ya mianzi na huhamisha kwa eneo mpya, haswa kwa kutarajia matunguzi, mafuriko, na maporomoko ya ardhi. Hii inaweza kuwa nadra katika nyakati hizi za kisasa, lakini roho ya bayanihan iko hai mioyoni mwa Wafilipino wanapotenda kama jamii moja huunga mkono kila mmoja wakati wa hitaji, hata inapochukuliwa kuwa haiwezekani kufanya hivyo.

Tunasherehekea kanuni hizi tunapojitolea kujenga na kufanikisha kanisa lenye mizizi ndani jamii, ambayo linakaribisha na linathibitisha dhamana takatifu ya watoto wote wa Mungu na linapanua ukarimu mwingi katika kujali ustawi wao, linafanya kazi kwa uaminifu kuwaweka kutoka kwa madhara yoyote.

Kwa kuathiri na kudhuru maadili yetu na wito wetu kama kanisa ni wito wa kuvunja au kuligawanya Kanisa la United Methodist, kuvunjilia mbali mali zake kisha kuzambaza kwa wahusika wakubwa zaidi. Mipango kama hii ni hatari kwa Mwili wa Kristo ambaye kupitia kwake waamini kuungamana kwa neema na kuishi katika uhusiano wa pamoja. Kuumiza sehemu moja ya Mwili wa Kristo dhidi ya mwingine pia inaumiza ushuhuda wetu kwa ulimwengu ulio na dhuluma na ukosefu wa haki.

Utangulizi wa katiba yetu unasema wazi kwamba kanisa "Ugawanyiko ni kizuizi kwa utume wake." Kwa hivyo, tunakubaliana na maaskofu wa Afrika na Ufilipino, ambao kwa maazimio tofauti, wametangaza upinzani wao mkubwa wa kulivunja na kugawanya kanisa.

Maadili Yetu:

Kushikilia kwa mvutano wenye neema tofauti kati yetu na kuvumiliana kila mmoja kwa upendo, twaangaza na tufikirie njia mpya za uhusiano wetu wa pamoja kwa Kanisa la United Methodist. Tunaangazia maadili haya ambayo yanasisitiza wito wetu:

1200x800_Unity_Hands_CrossFlames.jpg

Kushimu mipangilio ya muktadha kwa huduma.

 Huu ni mfumo na Jaribio la ujumuishaji wa huduma ambae ni ishara ya uwakili mwaminifu mbele za Mungu na ujumbe tofauti kwa ulimwengu unaobadilika. Heshima kama hiyo inamaanisha kwamba kanisa letu linahitaji kuelewa na kupata misemo tofauti na sahihi kwa muktadha ya huduma. Kufanya vinginevyo kunakuza uhusiano ambao kimsingi ni ukoloni.

 
rooted.jpg

Uhusiano unaounganisha kanisa kwa kutimiwa wito wake.

 Umoja wetu sio kwa umoja tu baali ni kwa kuueneza Injili inayofaa - kuwaalika wote kwa upendo wa Mungu na uhusiano kati ya mtu na jirani. Tunakaribisha na kudhibitisha kuwa wote ni watoto wa Mungu na kukumbatia kushiriki kwa kila mtu kuijenga jamii inayopendwa na Mungu.

UM_Books_1200x800.jpg

Usawa wa kisheria kwa majimbo ya kanisa.

 ikweli kuwa kuna utofauti kati yetu kwa mipangilio ya huduma. Kutimiza huduma yetu kwa pamoja kunaweza kuimarishwa kwa kutambua tofauti zetu za muktadha na kuruhusu kongamano la kati, kongamano ziliko umarekani, kongamano za majimbo (annual conference), au muundo wowote ulioundwa kufanya maamuzi na kuidhinishwa kwa kisheria na kongamano la pamoja la ulimwengu kushughulikia muktadha wetu wa huduma.

Wito Wetu:

Tuna nguvu pamoja. Kuwa katika huuma pamoja kama kanisa ulimwenguni huadhimisha umoja wetu katika utofauti na inathiri vyema mazingira tofauti tunayowakilisha. Wakati Utofauti ni changamoto, hatuamini mgawanyiko ndio njia sahihi ya kuponya majeraha ambayo husababisha maumivu kama Mwili wa Kristo. Kanisa la kweli lajitolea katika huduma kwa pamoja inajumuisha tofauti zake na inaruhusu kujitolea. Inaweza kupata msingi wa kawaida katika kudhibitisha jinsi tunavyofanya huduma madhubuti katika maeneo tunayohudumia.

Kutambua kwamba muktadha wetu tofauti zinahitaji suluhisho tofauti ni njia bora na inakuza utulivu. Njia hii inathibitisha ushuhuda wa kawaida wenye nguvu kwa jamii ya kimataifa. Neema ya Mungu iko kila mahali na kwa kila mtu. Tumeitwa kwa unyenyekevu kuitikia neema hii kwa kutambua matokeo yake mengi ulimwenguni.

Pendekezo Letu:

Kwa kuongozwa na kanuni na maadili yaliyotajwa hapo awali, na kugundua kuwa tunahitaji njia mpya ya kuwa katika uhusiano kwa neema kati yetu ili kutimiza utume tuliokabidhiwa na Yesu Kristo, tunapendekeza hatua zifuatazo na Mabadiliko ya sheria katika Kitabu chetu cha Nidhamu:

  • Kusimamishwa kwa vitendo vyote vinavyoashiria mpango wowote wa kuligawa au kutenganisha kanisa la United Methodist na kusambaza au kugawana mali za Kanisa.

  • Kuvumbua Mkutano wa Kanda ya Umarekani.

  • Kuanzisha usawa wa sheria kwa mamlaka ya mikutano ya kati.

Nyaraka za PDF zinapatikana kwa kupakuliwa

Bonyeza kiungo ili kupakua

  1. Utangulizi wa Agano la Krismasi

  2. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara